Home KITAIFA Mohamed: Sekta ya bahari ni biashara na inachangia uchumi kwa kiasi kikubwa

Mohamed: Sekta ya bahari ni biashara na inachangia uchumi kwa kiasi kikubwa

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika Wakala wa Meli Tanzania (TASAC ), Mohamed Salum amesema sekta ya bahari ni biashara na inachangia uchumi kwa kiasi kikubwa na kuna fursa mbalimbali.

Akizungumza leo, Julai,7 2025 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi huyo kwenye maonesho ya 49 Kimataifa ya Biashara Sabasaba amesema lengo la kushiriki Maonesho hayo ni kupata elimu na fursa zilizopo kwenye sekta baharini.

Amesema jukumu kubwa ni kusimamia mambo yanayohusu usalama wa bahari, meli, maeneo ya bandari na utekelezaji wa Mkataba wa Usalama wa Meli na maeneo ya bandari(ISPS Code).

“Kazi ya TASAC ni pamoja na kukagua vyombo vya usafiri majini, masuala ya kiusalama bandarini na kudhibiti uchafuzi wa mazingira majini unaosababishwa na vyombo vya usafiri majini,”amesema.

Pia amesema wananchi wanatakiwa kusoma masomo yanayohusu sekta ya bahari na kupata mafunzo ya kitaalamu ili kupata ajira lakini bado kuna changamoto ya kusoma masomo hayo.

“Hadi sasa bado kuna uhaba wa baharia duniani hivyo tunatakiwa kupata baharini wengi,”amesema.

Ameongeza kuwa wanasimamia shughuli za bandari kutoa vibali eneo linalofaa na lisilofaa kwa kujenga bandari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here