Home KITAIFA Rais Dk.Mwinyi atembelea banda la nishati maonesho ya Sabasaba

Rais Dk.Mwinyi atembelea banda la nishati maonesho ya Sabasaba

*📌Apatiwa elimu juu ya utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia

*📌 Wizara ya Nishati kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa tasisi zake kutekeleza majukumu yake kikamilifu

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

RaAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Julai, 7 2025 ametembelea banda la Wizara ya Nishati kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba jijini Dar es salaam

Akiwa kwenye banda la Wizara ya Nishati Dk.Mwinyi alipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Neema Mbuja, ambapo alimweleza juu ya hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwenye utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa nishati safi ya kupikia na kuongeza kuwa ajenda hiyo ni utekelezaji wa azimio la Mhe Rais Samia kama kinara wa nishati safi ya kupikia.

Amesema Wizara ya Nishati kupitia taasisi zilizopo chini ya Wizara zimekuwa zikitekeleza kwa vitendo ajenda hiyo kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambae ni kinara wa nishati safi ya kupikia kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia.

Wizara ya nishati tayari imezindua mikakati miwili ya nishati safi ya kupikia na ule wa mawasiliano ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here