Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
SHIRIKA la Uwakala wa Meli (TASAC) limesema kuwa Sekta ya Usafirishaji kwa njia ya maji inachangia uchumi mkubwa hivyo inahitaji kulindwa na kudhibitiwa.

Hayo ameyasema Julai, 5 2025 jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi hiyo Nahodha Mussa Mandia wakati alipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya 49 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba
Amesema kuwa njia ya Usafiri wa majini kinachoangaliwa ni usalama wa vyombo pamoja na mizigo inayoingia ndani pamoja na vyombo vidogo vya ndani vinavyotumia maziwa.
“Bodi tumejipanga katika kushauri katika kuona matokeo yanaonekana katika kuendelea kulinda usalama wa vyombo vya majini pamoja na abiria katika vyombo vidogo kwenye maziwa”amesema Nahodha Mandia.
Amesema kuwa katika usafiri wa bahari shehena kubwa zinazoingia ndio zinakwenda kuchochea uchumi wa nchi katika kuongeza pato la Taifa.

Nahodha Mandia amesema Serikali ya awamu ya Sita ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imeweza kuwekeza katika bandari mbalimbali na miradi hiyo itakuwa na matokeo mazuri katika katika kuendelea kuchochea maendelea kwa wananchi kwa uchumi wa mtu mmoja moja hadi taifa kwa ujumla .
Amesema katika Maonesho ya yanayoendelea wananchi watembelee Banda la TASAC kupata elimu kuhusu sekta ya usafiri wa majini.
Pia amesema wananchi wanatumia vyombi vidogo katika usafiri waangalie usalama wao kwa kuwa na vifaa vya uokozi.



