Home KITAIFA Rais Dk.Samia aipongeza TADB kwa utendaji mzuri

Rais Dk.Samia aipongeza TADB kwa utendaji mzuri

Na Esther Mnyika, Dodoma

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan  ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ( TADB) Kwa utendaji mzuri ulioleta tija kwa wakulima nchini. 

Ametoa pongezi hizo leo Agosti 8, 2025 Dk. Samia wakati wa kilele cha Maadhimisho  ya Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane ambapo kitaifa imefanyika Jijini Dodoma yameshirikisha  wakulima,  wafugaji na wavuvi kutoka mikoa mbalimbali nchini. 

Amesema utendaji mzuri  wa benki hiyo umewapa uwezo wa kuwezesha wananchi na kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa  TADB, Frank Nyabundege amesema  mtaji  wa benki hiyo umekua kutoka shilingi bilioni 60 hadi shilingi bilioni 442 pia amemshukuru Rais Dk.Samia  kwa kuendelea  kuwawezesha wakulima  ka kuwapatia mikopo ya pembejeo.

“Rais umeitafutia fedha Benki hii  kutoka kwa wahisani mbalimbali ambapo wakati unaingia madarakani hakukuwa na fedha kutoka kwa wahisani lakini tumepata shilingi bilioni 564 kupitia nguvu zako kutoka kwa wahisani mbalimbali katika diplomasia ya uchumi,”amesema.

Amesisitiza kuwa benki  hiyo itaendelea kudhamini  maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane  kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kwa sababu imiwezesha kuwa na mtaji mkubwa.

Nyabundege amesema wakati anaingia madarakani Rais Dk. Samia jumla ya mikopo ilikuwa shilingi trilioni 19  hadi  kufikia Juni mwaka huu shilingi trilioni 42.

“Hii maana yake kwamba uchumi wetu unakuwa na hiyo ni kwasababu ulivyoingia madarakani uliamua kwenda kufanya mageuzi katika nchi yetu kupitia sekta ya Kilimo na ndio maana ukatupatia sisi mtaji, na sisi tutaendelea kudhamini maonesho haya,”ameeleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here