Home KITAIFA TANESCO yanunua vitendea kazi kuboresha huduma kwa wateja

TANESCO yanunua vitendea kazi kuboresha huduma kwa wateja

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limenunua vitendea kazi  vya usafiri magari 100,  bajaji 100, na pikipiki 284 ikiwa  lengo ni kurahisisha na kuboresha huduma za usafirishaji na kuongeza ufanisi na utendaji kazi n kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.

Hayo ameyasema leo Septemba, 9 2025 jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja TANESCO,  Irene Gowelle amesema matokea yakununua vifaa hivyo yametokana na ziara iliyofanya na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo na kugundua kulikuwa na uhitaji wa vifaa hivyo.

“Kama Shirika tumekuwa tukitumia gharama kidogo kwenye ukodishaji wa vifaa hivi kwa ajili ya kutoa  huduma zetu ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita tulikuwa tukitumia takribani  ya shilingi bilioni 1.3  kila mwezi kwa ajili ya kukodisha vifaa hivi ambavyo vilikuwa vikitumika  kwa hiyo vifaa hivi vimenunuliwa kwa malengo na manufaa ya kuweza kurahisha upatikana wa huduma  kwa wateja wetu na kuweza kuwafikia kwa wakati,”amesema.

Ameongeza kuwa Vifaa hivyo vitaweka mazingira wezeshi na rafiki kwa wafanyakazi wao katika maeneo yote nchini kwenda kuwahudumia wateja ndani ya wakati na kwa muda.

Gowelle amesema uwepo wa vitendea kazi hivyo wanaamini utaenda kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wateja wetu lakini pia kuhakikisha kwamba lengo la serikali la kuhakikisha wateja wetu wanahudumiwa ndani ya wakati na wanapata huduma ya umeme ya uhakika.

Amesema usafiri huo baadhi  ya mikoa na wilaya nchini  umeshaaanza kutumika  hivyo kusaidia wateja kupata huduma ya umeme nchini kwa wakati.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here