Home KITAIFA Wanafunzi Milioni 1.17 wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la  saba kesho 

Wanafunzi Milioni 1.17 wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la  saba kesho 

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam 

JUMLA ya Wanafunzi 1,172,279 wa darasa la saba waliopo katika shule za msingi Tanzania Bara  jumla ya shule 19,441  wanatarajia kufanya mtihani  wa kumaliza elimu ya msingi kuanza kesho Septemba,10 hadi 11 2025.

Amesema kati yao wavulana ni 535,138 sawa na asilimia 45.65 na wasichana ni 637,141 sawa na asilimia  54.35.

Akizungumza leo Septemba, 9 2025 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Profesa Said Mohamed amesema kati ya watahiniwa 1,172,279 waliosajiliwa  kufanya mtihani mwaka 2025.

” Watahiniwa 10, 94,321 sawa na asilimia 93.35 watafanya  mtihani kwa lugha ya Kiswahili  na watahiniwa 77, 958 sawa na asilimia 6.65 watafanya  mtihani  kwa lugha ya kingereza ambayo wamekuwa wakitumia katika kujifunzia,”amesema Profesa Mohamed.

Ameongeza kuwa watahiniwa  wenye mahitaji maalumu  waliosajiliwa  kufanya mtihani huo ni 4,679 kati yao ni 92 wasioona,1,551 wenye uono hafifu, 1,079 wenye uziwi, 448 ni wenye ulemavu wa akili na1,509 wenye ulemavu wa viungo.

Profesa Mohamed ameeleza kuwa  katika mtihani wa kumaliza  elimu ya msingi  nijumla ya masomo sita ambayo ni Kiswahili, English Language, Sayansi na Teknolojia/Science, Hisabati, Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi pamoja na uraia.

Pia amezitaka shule na wanafunzi wote kuepuka vitendo vya udanganyifu, likisisitiza kuwa halitasita kufuta matokeo ya yeyote atakayebainika kushiriki katika vitendo hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here