Home KITAIFA Wizara ya Utumishi inaandaa muswada wa sheria mpya kuwajibisha watumishi wanaojihusisha rushwa

Wizara ya Utumishi inaandaa muswada wa sheria mpya kuwajibisha watumishi wanaojihusisha rushwa

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema Wizara yake inaandaa muswada wa sheria utakaopewa mamlaka ya kuwajibisha watumishi wa umma wa ngazi ya nchini wanaojihusisha na rushwa.

Pia amesema serikali itaendelea kuhakikisha mchakato wa kupata ajira katika taasisi, idara na mashirika ya umma unakuwa ni wa uwazi na unaozingatia misingi ya ushindani kama inavyoelekezwa na sera ya ajira nchini.

Kauli hiyo ametoa leo Disemba,12 2025 jijini Dar es Salaam Ridhiwani amesema kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba la Disemba, 11 mwaka huu kufanya mapitio ya sheria ili kuhakikisha watumishi wa ngazi ya chini wanaojihusisha na rushwa wanawajibishwa.

“Marekebisho haya yanahitajika kwani sheria ya sasa hayajumuishi kundi hili la watumishi na muswada huu utapanga makundi ya watumishi kulingana na nafsi zao ili kuwezesha kuwawajibisha ipasavyo,”amesema.

Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha wa 2025/26 serikali imetoa vibali vya ajira 41,500 ikiwemo nafasi za ajira 12,000 kati ya idadi hiyo ya nafsi za ajira nafsi 5,000 ni za kada ya afya na 7,000 ni kada ya ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati.

Amesema kuwa usaili wa nafasi hizo unatarajia kuanza Disemba,13 2025.

Kikwete akizungumzia kuhusu watumishi amesema watumishi wa umma wazembe na wasiofanyakazi hawatakuwa na nafasi katika serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassani.

Amesema jambo la watumishi wa umma kufaya kazi kwa mazoea limefika mwisho na kusisitiza kuwa kwa sasa hakuna muda wa kucheza cheza bali ni kufanya kazi kwa maslahi ya umma.

Amesema linapofika katika jambo la utendaji kazi kama haliwezekani aambiwe mapema na kuwataka watumishi kuacha nidhamu ya uwoga kwa kusema atafanyakazi ambayo haiwezekani kwa muda huo.

“Nataka kusema wazi sitawavumilia watumishi wa umma wenye nidhamu ya uwoga, kama kuna jambo umepewa haliwekani kuwa muwazi kusema kuwa haliwezekani na si kukubali kisha baadae kushindwa kulifanya na kutoa majawabu.

“Mabadiliko ndani ya utumishi wa umma yatatekelezwa, tuvumilianetu kwani watumishi hawa wa umma mnaowataka ninyi kuwa nao kijiweni watakuwepo huko hivi karibuni, kama kuna mtu aamini haya basi ajaribu na sitaruhusu mtu kuja kumuombea mtu radhi, kwa sababu akikosea amekosea na hatutavumilia katika hilo,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here