Home KITAIFA RAIS DK.SAMIA:AONGEZA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI KWA ASILIMIA 35.1

RAIS DK.SAMIA:AONGEZA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI KWA ASILIMIA 35.1

Singida

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa mwaka huu Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1% ambapo kwa ongezeko hili sasa kima cha chini kitapanda kutoka 370000 hadi 500000.

Akizungumza Mei 01,2025 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoani Singida, Rais Dk.Samia amesema Mwezi Mei mwaka jana wakati wa Siku ya Wafanyakazi Serikali ilieleza ugumu wa uchumi ulivyokuwa wakati ule na kuwasihi wasiongeze gharama kwa Serikali kwa kuongeza mishahara bali waliendelea na upandishaji wa madaraja na kutoa maslahi mengine ya wafanyakazi.

“Sasa kwa mapenzi makubwa na kwa namna mlivyoiunga mkono Serikali ilipowaomba mfunge mkanda na mkaamua kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kufanya uchumi wetu ukue kwa 5% mwaka huu, kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Wafanyakazi oyeee, miamvuli oyee, naona miamvuli imepanda sasa wakati wote ilikuwa chini sasa imepanda.

“Sasa kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Mimi na wenzangu na baada ya kuangalia uchumi ulivyopanda na umepanda kwasababu ya nguvu zenu Wafanyakazi, ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1%, Wafanyakazi oyeee,”amesema.

Amesema nyongeza hiyo itakayoanza kutumika mwezi Julai mwaka huu itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 370000 hadi shilingi 500000, ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiwango kizuri jinsi bajeti inavyoruhusu lakini nataka niwaambie nyongeza nzuri ipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here