Home KITAIFA KIKWETE : WATU WENYE ULEMAVU NAO NI SEHEMU YA NGUVU KAZI...

KIKWETE : WATU WENYE ULEMAVU NAO NI SEHEMU YA NGUVU KAZI YA TAIFA

Dodoma

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete amewakumbusha Watu wenye Ulemavu kuwa nao ni sehemu ya nguvu kazi ya Taifa hivyo wanapaswa kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo sawa na wasio na ulemavu na hiyo imekuwa dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Hayo ameyasema Mei,9 2025 jijini Dodoma na Kikwete wakati wa Kongamano la watu wenye ulemavu kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar lililoandaliwa na Ikupa Trust Fund akimuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Mashaka Biteko kwenye kongamano hilo.

“Nawahakikishia washiriki utayari wa serikali kushirikiana nao katika nyanja mbali mbali ikiwemo kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kushiriki shughuli zote za kijamaa ikiwemo kujenga uchumi na kujenga Jamii itakayopambana kwa ajili ya maslahi mapana ya Wenye Ulemavu,” amesema.

Kikwete amepokea mchango wa shilingi milioni moja kutoka kwa watu wenye ulemavu kwa ajili ya uchukuzi wa fomu ya kugombea Urais ya Dk.Samia Suluhu Hassan kwenye Uchaguzi Mkuu unaotajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Katiika hatua nyingine Kikwete amekabidhi vifaa wezeshi kwa makundi hayo ya watu wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni nane ambavyo ni mafuta chupa 103, miwani ya jua 38, Magongo 91, Fimbo nyeupe kwa wasioona 36 na Kofia 27.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here