Home SIASA Makalla: ccm itaendelea kutatua kero za wananchi

Makalla: ccm itaendelea kutatua kero za wananchi

•Aongea na wananchi DUMILA na kusikiliza kero

Morogoro

KATUBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi(CCM) CPA, Amos Makalla amesema chama hicho, ndicho chenye jukumu la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili Watanzania.

CPA, Makalla amesema wajibu huo unatekelezwa vema na CCM, akiwataka Watanzania kutokuwa na wasiwasi kuhusu utatuzi wa kero zinazowakabili kwa sababu maendeleo yanaendana na changamoto.

Ameeleza hayo leo Mei, 16 2025 katika Kata ya Dumila wilayani Kilosa aliposimama kuwasalimia wananchi wa eneo akieleke wilayani Gairo kufanya mkutano wa hadhara.

“CCM ndio yenye thamana ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wengine hawawezi hilo,” amesema CPA.

Katika mkutano huo, Makalla alizibeba kero za maji, barabara, ushuru na stakabadhi gharani zilizowasilishwa na wananchi wa Dumila aliyewapa fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here