Home KITAIFA Khamis: Ameitaka TASAC kuendelea kutoa elimu kwa wananchi

Khamis: Ameitaka TASAC kuendelea kutoa elimu kwa wananchi

Dodoma

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amelitaka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu madhara ya kutupa taka baharini, maziwa na mito.

Hayo ameyasema Juni, 4 2025 jijini Dodoma alipotembelea Banda la TASAC katika Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2025 yanayofanyika kuanzia tarehe 01 – 05 Juni, 2025.

Amesema TASAC waendelee Kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri majini ili kujua namna wanavyodhibiti taka zinazotokana na vyombo vya usafiri majini.

“Kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya watu kutupa taka baharini ili kuona itakuwaje bila kujua madhara yake baadala ya kutupa kwenye dustbin. Ninawaasa waendelee kuwapa wananchi elimu ya kutunza mazingira ya maji,” amesema Khamis.

Ameongeza kuwa ameona juhudi zao katika kutunza vyanzo vya maji kwa kuzingatia kuwa kuna vyombo vidogo vyenye shughuli nyingine ikiwemo uvuvi na zina mambo mengi yanayoweza kuchafua mazingira ya bahari ambayo anaimani TASAC wanahusika nayo.

“Muone jinsi ya kushughulikia vyombo hivyo sababu kwa namna moja ama nyingine zinaleta athari katika maji. Inawezekana shughuli hizo zikawa ni uvuvi kwahyo muangalie namna ya kuvidhibiti visifanye uchafuzi,”amesema.

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi wa TASAC,Martha Kelvin amesema majukumu makubwa wanayofanya ni pamoja na udhibiti na usimamizi wa Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa Mazingira Majini.

Amesema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ili kuonesha TASAC wanavyotunza mazingira ya maji.

“Jukumu letu sisi TASA ni pamoja na kakagua vyombo vya usafiri majini, na katika kaguzi zetu tunahakikisha kila chombo cha abiria au mizigo kinakiwa na sehemu ya kuwekea taka ili kuhakikisha bahari, maziwa na mito inakuwa salama bila kuathiriwa na taka zitokanazo na vyombo hivyo vya usafiri majini,” amefafanua.

Amesema pia wanatoa elimu kwa waendesha vyombo vya usafiri majini jinsi ya kupambana na umwagikaji wa mafuta katika bahari, maziwa na mito hivyo wanahakikisha kwa namna yoyote hawachafui mazingira ya maji ili kulinda viumbe vilivyopo kwa maslahi wa Taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here