TARAKEA- ROMBO
KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla amesema uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya ni mzuri na ni wahisistoria kutokana na mataifa hayo kutegemeana katika shughuli za biashara na kichumi.

Makalla ameeleza hayo leo Juni 9,2025 wakati akihutubia mkutano hadhara katika eneo la Tarakea wilayani Rombo mkoani Kilimanyaro akipomgeza marais wa nchi mbili Dr samia Suluhu na William Ruto kwa kuendelea kuimarisha mahusiano ya nchi mbili na kuchochea kukua kwa Biashara.
Amesema kuna muingiliano wa biashara kati ya mataifa hayo mawili kwani kuna wakenya wanaokwenda kulima viazi Rongai na Watanzania wanakwenda kulima Kenya, pia wanategemeana katika biashara zikiwemo za mbogamboga.

Pia Makalla amewapongeza viongozi wa mataifa hayo mawili kwa kuendelea kulinda na kuimarisha uhusiano mzuri uliopo ambao ulijengwa na waasisi wa mataifa hayo mawili, kwani kutegemeana kwao kunachagizwa na amani na utulizu uliopo.

Makalla amewataka wananchi wa eneo hilo ambalo ni mpakani kuwa mabalozi wazuri kwa kushirikiana na wakenya vizuri kwa sababu mataifa hayo yanategemeana na kutegemeana huko kunachagizwa na amani na utulivu uliopo katika mataifa.