Home KITAIFA Majaliwa kuzindua Samia Legal Aid Juni, 16 Dar es Salaam

Majaliwa kuzindua Samia Legal Aid Juni, 16 Dar es Salaam

-Ataka wananchi wajitokeze kwa wingi hususani wale wenye changamoto za maswala ya kisheria.

Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid) inayotarajia kufanyika kuanzia Juni 16 hadi 25, 2025. kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za kisheria ikiwemo migogoro ya ardhi na masuala ya ukatili wa kijinsia.

Kampeni hiyo inafanywa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkoa wa Dar es salaam na Wizara ya Katiba na sheria kwa udhamini wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia na inafahamika kama Mama Mama Samia Legal Aid Campeign ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa katika viwanja vya Maturubai Mbagala Wilaya ya Temeke jijini humo

Akizungumza leo Juni, 13 2025 jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila amesema lengo la kampeni hiyo ni kuwasaidia wananchi kushughulikia kero na changamoto za kisheria ili kuleta haki,usawa,amani na maendeleo hivyo amewataka wananchi wenye changamoto za kisheria kujitokeza

“Kampeni hiyo ya msaada wa sheria ya Mama Samia itazinduliwa juni 16,2025 kwenye uwanja wa maturubai Mbagala jijini humo na baada ya uzinduzi kampeni hiyo itakwenda kwenye wilaya zote za Mkoa huu na wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi,”amesema.

Amesema ndani ya jiji hilo mbali na migogoro ya ardhi kumekuwa na matukio ya ukatili wa kijinsia hivyo kutakuwa na wataalamu wa sheria na madawati ya kijinsia ili lengo la Rais Dk.Samia kuendesha kampeni hiyo iweze kufanikiwa.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa huduma za kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ester Msambazi amesema kuwa kampeni hiyo imeanza kutekelezwa mwaka 2023 na imefika kwenye mikoa mitano ya Visiwani na Bara mikoa 25 ya Tanzania bara ikiwa tayari imefikia na kusaidia zaidi ya wanancni milioni 2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here