Home KITAIFA Polisi Tanga yasarambatisha genge tishio la watoto wa ibilisi

Polisi Tanga yasarambatisha genge tishio la watoto wa ibilisi

Na Boniface Gideon, Tanga

JESHI la polisi mkoani Tanga, limewakamata watu watano wanaofahamika kama ‘Watoto wa Ibilisi’ wanaojihusisha na matukio ya uhalifu Jijini Tanga ikiwemo kumjeruhi na kumibia simu Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari Popatlal mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Leo Juni 18 2025, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, ACP Almachius Mchunguzi amesema vijana hao walikamatwa Juni 15 mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga baada ya jeshi Hilo kufanya operesheni na misako katika maeneo mbalimbali.

Amesema vijana hao walimjeruhi vibaya Mwalimu huyo aliyefamika kwa jina la Katwibu Siraji ambaye walimpora Simu wakati akitoka msikitini kuswali.

“Bahati mbaya mimi sipendi watu watumie neno ‘watoto wa ibilisi’ kwasababu Ibilisi hakuwahi kuwa na mtoto,” amesema Kamanda alipoulizwa kuhusu kukamatwa kwa watoto hao ambao wamekuwa wakifanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Tanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here