Home SIASA Madai sita ya ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu

Madai sita ya ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

KUELEKEA kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba Mwaka huu,Chama Cha Act Wazalendo kimeendelea kusisitiza madai sita ikiwemo Makamishna wa Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi(INEC)wapatikane kwa ushindani,huku Wakurugenzi wa Halmashauri wasiwe wasimamizi wa uchaguzi kwenye Majimbo.

Pia mawakala wafanye shughuli zao bila kubughudhiwa na wasizuiwe kwa namna yoyote ile,wagombea wote wasienguliwe ili wananchi wapewe nafasi ya mwisho kuamua viongozi wanaowataka, na pasiwepo na kura feki,pamoja na Vyombo vya Ulinzi na usalama kutoingilia mchakato wa uchaguzi. 

Madai hayo yametolewa leo Juni 21,2025 Jijini Dar es salaam na Kiongozi wa Chama hicho Dorothy Semu,wakati wa Uchambuzi wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2025/2026 uliyofanyika Makao Makuu ya Chama hicho Magomeni,Kinondoni.

Dorothy Semu ambaye pia ni Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho amesema kwamba Act Wazalendo inasisitiza yale yanayoitwa mabadiliko ya Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) hayapindishwi na yatoe mabadiliko ya kweli yatakayohakikisha kwamba unafanyika uchaguzi huru,haki na wenye kuaminika. 

Akizungumzia kuhusu fedha zilizotengwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu 2025, Kiongozi huyo amedai kuwa Chama hicho kinataka bajeti iliyotengwa kwa ajili ya uchaguzi itumike kudumisha kuleta uchaguzi huru,haki nawa kuaminika na isitumike kuharibu demokrasia wakati wa uchaguzi.

“Serikali imetenga takribani shilingi trioni 1,kwa ajili ya uchaguzi mkuu,ambapo hadi sasa inadai imetumia shilingi Bilioni 741.5 ,na shilingi bilioni 378.2 inaelezwa kutengwa kwa ajili ya kuwezesha mchakato wa uchaguzi kwa mwaka 2025,”amesema Semu 

“Fedha hizi zilizotengwa na zinazotumika kwa ajili ya uchaguzi ni fedha zetu sisi wananchi,sio fedha za chama chochote kile,tumeshuhudia namna ambavyo uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na Vitongoji mwaka 2024 zilitumika shilingi bilioni 254.82 na zilitumika kuendelea kuvunja demokrasia tuliona ambavyo fedha hizi ziliteketea nabadala ya kutumika kudumisha demokrasia,kumpa Mtanzania haki yake ya kuchagua viongozi,zilitumika kupora haki na demokrasia kuchagua viongozi wetu,” ameongeza

Aidha ameeleza kuwa kwa mwaka mwingine tena,vyama vya siasa vinaenda kwenye uchaguzi mkuu,vikiwa bado havina uhakika wowote kwamba kutakua na haki,na misingi ya demokrasia itaheshimiwa na kuzingatiwa. 

Amesema Act Wazalendo kimeamua kuingia kwenye uchaguzi huu kikiwa na ali ya kimapambano,na ali ya kuendelea kulinda thamani ya kura na kuhakikisha ustawi wa Wananchi wa Watanzania. 

“Act Wazalendo tunaendelea kusisitiza kwamba hatutaki fedha hizi zitumike kuwaumiza wananchi,hatutaki fedha hizi zitumike kupora maamuzi ya Wananchi,tunataka uchaguzi huru,wa haki ambapo vyama vyote vitapata haki sawa na Uwanja sawa wa kueleza wananchi kipi chakufanya bila bugudha,”amesema. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here