Home UCHUMI EADB yatoa bilioni 63.2 kuiwezesha taasisi za fedha Tanzania

EADB yatoa bilioni 63.2 kuiwezesha taasisi za fedha Tanzania

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

BENKI ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imesaini hati ya makubaliano matatu ya kifedha na taasisi zinazoongoza fedha nchinii kwaajili ya utoaji mitaji jumla ya shilingi bilioni 63.2 ili kuchochea SMEs,Makazi na ukuaji wa uchumi.

Akizungumza leo Juni, 23 2025 jijini Dar es Salaam baada ya kusaini Makubaliano hayo Kamishina wa Maendeleo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Charles mwamaja amesema fedha hizo zenye lengo la kukuza ukuaji wa uchumi, kusaidia biashara ndogo na za kati (SMEs) na kushughulikia upungufu wa makazi ya nchini .

“Taasisi zilizonufaika na mpango huo ni pamoja na Benki ya Maendeleo ya TIB ambayo imewezeshwa kwa mtaji wa shilingi bilioni 30, Azania Bank iliyopewa shilingi bilioni 13.3, na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba (TMRC) ambayo imepata shilingi bilioni 20 kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kutoa mikopo ya nyumba,”amesema.

Amesema uwezeshaji huo ni kuleta mabadiliko ya haraka ya kiuchumi, kuongeza ujumuishaji wa kifedha na kuweka mazingira wezeshi kwa Watanzania wengi kunufaika na huduma za kifedha.

Amesema kuukopesheka kwa miradi ya kimkakati kwa ajili ya kuwezesha kutoa mikopo kwa taasisi za fedha kujenga nyumba zenye gharama nafuu.

Ameongeza kuwa Watanzania wafahamu kuwa kuna fedha Benki ya maendeleo na azania Benki wamepata mikopo hiyo wahudumiwe wajasiriamali na kuwawezesha kupata mkopo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa EADB, Bernard Mono, amesema fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za nishati, uzalishaji viwandani, miundombinu na madini, ambazo zina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amesema SMEs kwa ujumla ni injini ya uchumi lazima kuwwsaidia katika kuleta ajira na kukuza uchumi na Tanzania imenufaika kwa kiasi kikubwa.

Baadhi ya wanufaika wa makubaliano hayo wamesema hatua hiyo ni chachu ya kuongeza kasi ya upatikanaji wa mitaji, kupanua huduma za kifedha na kuendeleza ajira kwa Watanzania, hususan vijana, kupitia shughuli za kiuchumi zinazofadhiliwa na mikopo hiyo.

Uwekezaji huu wa EADB unatajwa kuwa sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo kusaidia ukuaji wa uchumi wa kikanda kwa kuimarisha mifumo ya kifedha ya ndani, pamoja na kuchochea maendeleo endelevu katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here