Home KITAIFA Chalamila:Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuhakikisha wananchi kulinda miundombinu ya umeme katika...

Chalamila:Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuhakikisha wananchi kulinda miundombinu ya umeme katika mitaa yao.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri  ya Ubungo na Kinondoni kuhakikisha wanasimamia wananchi katika mitaa yao kulinda miundombinu ya umeme kwa maslahi ya taifa.

Hayo ameyabainisha leo Juni 24,2025 jijini Dar es salaam wakati wa kikao kazi cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri hizo.

Amesema katika mkoa huo kuna miradi mbalimbali mikubwa ya umeme imejengwa hivyo wanapaswa kuwa wazalendo katika kuilinda.

“Umeme ni ajira,umeme ni maisha  pia kuchangia Pato la Taifa hivyo tunapaswa kuwa wazalendo katika kuitunza miundombinu yake kwa maslahi binafsi na nchi yetu hivyo kuacha kutumia muda mwingi kuzungumzia madili,”amesema Chalamila.

Ameongeza kuwa wenyeviti wa mitaa wanaongoza jopo kubwa la wananchi katika mitaa yao hivyo dhamana ya ulinzi na amani ipo mikononi mwao.

“Tunapozungumzia amani ya Taifa letu inatokana na utulivu wa taifa letu lakini amani ya pili inatokana na uwepo wa huduma za kijamii ikiwemo umeme vinapokosekana utulivu hauwezi kuwepo,”‘amesema.

Chalamila amewataka wenyeviti hao kuyasema mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi wao ili waweze kuyafahamu hali itakayowapelekea kuzidi kuendeleza amani iliyopo na kuendelea kujenga imani kwa Rais.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando ameahidi kushirikiana na wenyeviti wa serikalinkutekeleza kwa wakati maagizo ya serikali na chama na kuahidi kushughulikia kwa haraka changamoto na kero za Tanesco pindi  zinapojitokeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange amesema shirika hilo kwa kutambua Wenyeviti wa Serikali za mitaa ni wadau muhimu likaona liandae kikao kazi kwa ajili yao ili kutengeneza mfumo mzuri wa mawasiliano ambao utawasaidia kujua wananchi wanasemaje kuhusu huduma za Tanesco.

Amesema wameandaa kikao hicho ili  wenyeviti wawe na uwezo wa kuelewa nini kinafanywa na shirika hili na kwamba elimu watakjaoipata waweze kuitumia kuwaelimisha wananchi walioko katika maeneo yao.

“Hivi karibuni  kulifanyika Mkutano wa Nishati nchini Urusi ambapo tumeelekezwa kuunganisha umeme watu milioni 1.7 kwa mwaka wakata sasa tunaunganisha umeme  watu laki 500000 hadi 600000 kwa mwaka  sasa tutafuata watu kwaajili ya kuunganisha umeme tofauti na kipindi cha nyuma walikuwa wanatufuata wao ili  kufikia malengo,”amesema.

Mbali na utoaji wa elimu hiyo,  Twange amemkabidhi Chalamila na viongozi wachache wa mitaa Jiko la Umeme ambalo linatumia umeme kidogo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here