Home SIASA Wasira: CCM hatutaki mgombea ila tunateua wachache kati ya wengi

Wasira: CCM hatutaki mgombea ila tunateua wachache kati ya wengi

Na Mwandishi wetu, Mwanza

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira amesema kazi iliyobaki baada ya kuvunja Bunge ni kuendesha taratibu za namna ya kupata wagombea ubunge na kwamba Chama hicho hakitaka mgombea ila kitateua mmoja kati ya wengi.

Wasira ameyasema hayo leo Juni 24,2025 alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wakati kihitimisha ziara yake katika mkoa huo.

“Kazi iliyobaki kwa CCM baada ya kuvunja Bunge ni kuendesha taratibu za namna ya kupata wagombea ubunge na sisi tumesema wanachama wetu wanaotaka ubunge wako wengi lakini sisi tunataka mgombea mmoja kwa kila jimbo.

Sasa tumesema wagombea wengi lakini tutajucha na wala hatuwakati tunateua , unajua tofauti ya kuteua na kukata? Ukikata unakata kwa hasira ukiteua unatazama uwezo kwa wakati,”amesema

Ameongeza kuwa wao hawakati mtu ila wanateua wagombea wachache kati ya wanachama wengi wale wanaobaki watasubiri tena ,wengine ni vijana watasubiri.

“Wanajua Juni 28 wanagombea wanaleta fomu, Julai 2 wanarudisha fomu kwa heshima tu halafu wakimaliza vikao vyetu vitawatizama tazama na kupendekeza na tunataka kupendekeza wagombea ambao wanakubalika na wananchi,”ameeleza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here