Home SIASA Asenga leo Juni,28 achukua fomu ya kuwani Ubunge kipindi cha pili

Asenga leo Juni,28 achukua fomu ya kuwani Ubunge kipindi cha pili

Na Mwandishi wetu, Morogoro

MBUNGE wa Jimbo la Kilombero kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abubakar Asenga leo Jumamosi Juni 28, 2025 amechukua fomu ya kuwania Ubunge kwa kipindi kingine cha pili katika Jimbo hilo lilopo Mkoani wa Morogoro.

Asenga amechukua fomu hiyo na kutimiza masharti yote muhimu majira ya saa 07: 48 asubuhi.

Kulingana na duru mbalimbali za habari, Asenga ndiye Mgombea wa kwanza kuchukua fomu hiyo kwa upande wa Tanzania bara, baada ya dirisha hilo kufunguliwa nchi nzima hii leo Juni 28, 2025 kwa wagombea wa Udiwani na Ubunge kwa Tanzania bara.

Asenga kama zilivyokuwa zimetangazwa taratibu za Chama chake, ameonekana kwenye Ofisi za CCM akiwa peke yake bila ya wapambe ama misafara ya watu na vyombo vya usafiri ikiwa ni utekelezaji wa marufuku iliyokuwa imeweka na Chama hicho.

Ni miongoni mwa wabunge wengine wanaotarajiwa kumaliza utumishi wao wa Kibunge rasmi Agosti 3, 2025 Bunge la 12 litakapovunjwa rasmi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here