Home SIASA Dk.Njama Kuwania Jimbo la Kibamba

Dk.Njama Kuwania Jimbo la Kibamba

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MTUMISHI wa Idara ya Afya katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Dk. Ally Njama, amejitokeza kuchukua fomu ya  kutia nia kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba.

Dk. Njama, historia yake katika kutimiza majukumu ya kichama na Serikali, inaonesha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa na pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha kada huyo wa CCM, aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi katika Hospitali ya Mwananyamala kwa miaka minne na aliwahi kuwa Mjumbe wa Bodi wa Shule ya Sekondari Kambangwa iliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pia ni Mjumbe wa Chama Cha Serikali za Mitaa (TALGU)  na alikuwa Mjumbe wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) akitumikia vipindi vitatu.

Kutokana na uzoefu huo, mwanachama huyo, anakiri kwamba anaweza kuliongoza Jimbo la Kibamba ikiwa jina lake litarejeshwa kuwania nafasi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here