Home SIASA Dk. Walter achukua fomu kuwania jimbo la Kibamba

Dk. Walter achukua fomu kuwania jimbo la Kibamba

Sophia Kingimali, Dar es Salaam

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.Walter Nnko, amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika Jimbo la Kibamba.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo Juni 29, 2025 ameweka wazi kuwa amechukua jukumu hilo ili kutimiza ndoto yake kupitia siasa.

Dk.Nnko, katika historia yake kwenye siasa kupitia CCM, mwaka 2022 alifanikiwa kushika nafasi ya pili MNEC Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia alishika nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya na sasa amechukua fomu ili kutia nia kuwania Jimbo la Kibamba.

Leo sina mengi ya kusema kwa maana huu ni mchakato wa kwanza, hivyo hatua nyingine zinaendelea nikifanikiwa jina langu kupita nitaeleza mengi kuhusu dhamira iliyonisukuma kutia nia kuwania ubunge katika jimbo hili la Kibamba” amesema.

Zoezi wa uchukuaji na urejeshi wa fomu za ubunge,udiwani na viti maalum lilianza rasmi Juni, 28 2025 ambapo wagombea wanafsi hizo wanaendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here