Home KITAIFA Miradi ya Nishati Safi iache alama kwa wananchi-Kamishna Luoga

Miradi ya Nishati Safi iache alama kwa wananchi-Kamishna Luoga

📌Afungua Mkutano wa Sita wa Kamati ya Uwekezaji miradi ya nishati safi ya kupikia

📌 Aishukuru EU na UNCDF kutekeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo

📌 Asema ushirikishwaji wa srkta binafsi ni chachu ya kuleta maendeleo miradi ya nishati safi

📌UNCDF kuangalia uwezekano wa kituo cha elimu kwa vitendo kuhusu nishati safi ya kupikia

Na Mwandishi wetu

KAMISHINA wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amesema utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia inapaswa kuweka alama kwa wananchi ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

Kamishna luoga ameyasema hayo leo julai 3 ,2025 wakati akifungua mkutano wa sita wa wa kamati ya uwekezaji miradi ya nishati safi ya kupikia unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali, Umoja wa Ulaya na Shirika la umoja wa mataifa la maendeleo na mitaji ili kusaidia utekelezaji wa miradi ya nishati safi ya kupikia

‘’Serikali kupitia Wizara ya Nishati na wadau wa nishati safi ya kupikia imefanya kazi kubwa kuhakikisha malengo yanatimia ikiwemo utekelezaji na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye miradi ya nishati safi ya kupikia ili kubadili fikra na kutimiza azma ya Serikali ya kufikia asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo 2034, ’’ amesema Mhandisi Luoga.

Amesema chini ya uwepo wa kamati hii ya uwekezaji kumekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo uwekezaji kwenye teknolojia mbalimbali za miradi ya nishati safi ya kupikia ili kuwezesha wanachi kutumia teknolojia mbalimbali ikiwemo gesi,umeme, na mabaki ya kinyesi cha wanyama na kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi.

Kwa upande wake, Mratibu wa mradi kutoka UNCDF Bw. Emmanuel Muro amesema UNCDF kupitia Cook fund chini ya ufadhili wa Umoja wa ulaya inaandaa mpango wa kuanzisha kituo maalum cha matokeo kwa vitendo ili kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa nishati mbalimbali zinazotumika kwa ajili ya matumizi ya kupikia ili wananchi wawe na uwelewa mpana juu ya nishati mbalimbali za kupikia.

Mkutano huo wa sita wa wadau umepitisha wafanyabiashara wadogo 17 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya teknolojia ya nishati safi ya kupikia kwa ajili ya ufadhili ili isaidie urahisishaji kwa watumiaji wa teknolojia ya nishati safi ya kupikia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here