Home KITAIFA Nishati safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia Wizara inatekeleza kwa...

Nishati safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia Wizara inatekeleza kwa vitendo-Dk.Kazungu

๐Ÿ“ŒApokea Magari Mawili kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuanza kampeni ya kutoa elimu ya uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia nchi nzima

๐Ÿ“Œ Amshukuru Dk. Samia kwa kuwa kinara wa nishati safi na kuibeba ajenda hiyo

๐Ÿ“Œ Umoja wa Ulaya waridhishwa na jitihada za Tanzania kwenye kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia

๐Ÿ“ŒUNCDF yaahidi kushirikiana na Wizara kuhakikisha watanzania wanafikiwa na elimu ya nishati safi

Na Mwandishi wetu

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati Jadidifu, Dk. Khatibu Kazungu leo 04 Julai, 2025 amepokea magari mawili yatakayotumika kwa ajili ya kampeni ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia chini ya kampeni ya nishati safi ya kupikia Okoa Maisha na Mazingira itakayoendeshwa nchi nzima na Wizara ya nishati kwa kushirikiana na UNCDF.

โ€˜โ€™Ajenda ya Nishati safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia na sisi Wizara ya Nishati tuko tayari kwa utekelezaji ili kumuunga mkono Mhe. Rais Samia,โ€™โ€™ amesema Dk. Kazungu.

Aidha, ameishukuru Umoja wa Ulaya, na UNCDF kwa kutekeleza mradi wa nishati safi ya kupikia chini ya mfuko wa Cook fund kwa kuwa umesaidia kubadili maisha na mitazamo ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya Nishati safi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Balozi wa Umoja wa Ulaya, Balozi Christine Grau amesema umoja wa Ulaya uko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye utekelezaji wa Nishati safi ya kupikia na tayari EU imetoa kiasi cha Euro Milioni 19.4 sawa na shilingi Bilioni 59 kutekeleza miradi ya nishati safi ya kupikia kwa mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro na Mwanza.

Kuhusu magari amesema magari hayo mawili yana thamani ya Euro 130,000 na amewataka wizara ya Nishati kuhakikisha wananchi wa vijijini wanafikiwa na nishati safi ya kupikia.

Tanzania inajipanga kutekeleza kwa vitendo mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia chini ya mkakati wa Mawasiliano wa Taifa ili kutoa elimu kwa wananchi na kufikia lengo la Serikali la asilimia 80 ya watanzania kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here