Home KITAIFA UDOM yaja na mashine ya teknolojia ya uuzaji vimiminika kidigitali

UDOM yaja na mashine ya teknolojia ya uuzaji vimiminika kidigitali

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

CHUO Kikuu Dodoma (UDOM) kimekuja na mashine ya teknolojia ya uuzaji wa vimiminika kidigital ambapo imekuja kutatua changamoto mbalimbali za wajasiliamali lakini pia kuokoa muda.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 49 ya biashara Sabasaba jijini Dar es salaam julai 3,2025 muhazili Mwandamizi kwenye ndaki ya sayansi za komputa na elimu angavu kutoa UDOM Hassan kilavo amesema kufuatia kasi ya ukuaji wa teknolojia ndio umepelekea chuo hiko kubuni mashine hiyo ya kuuzia vimiminika.

“Hii ni teknolojia ni mpya hapa kwetu tumeianzisha mahususi kwa ajili ya wafanyabiashara wa vimiminika kwani kwa kutumia mashine hii utaweza kuokoa muda na haiitaji muhudumu kwani inaweza kusetiwa na mtu akajihudumia mwenyewe”,amesema

Aidha amesema mashine hiyo inatoa huduma ya kidigital kwani inamifumo ya malipo ya kidigital ambapo haiitaji mtu kuwepo ili kupata huduma badala yake mteja anaweza kujihudumia mwenyewe

Ameongeza kuwa ikiwa mjasiliamali anamtaji wake lakini hana mashine wanaweza kuingia makubalino na kumpatia mashine kwa mkopo au kwa maelewano maalumu.

Amesema kama mtu hana milioni 14 ya kununulia wanaweza kukaa chini na kuongea waone namna ambavyo wanaweza kuweka mikakati ya kulipia mashine hiyo.

“Niwaambi wajasiliamali Sasa hivi tunaenda kiteknolojia zaidi kwa hiyo watu watumie keknolojia kwa ajili ya kurahisisha mambo wanayoyafanya.

Mashine hiyo yakuuzia vimiminika imetengenezwa watumishi wa Chuo Kikuu Cha UDOM ambapo zinatengenezwa kutokana na uhitaji wa mtu na aina ya vimiminika vinavyotarajiwa kuuzwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here