Home KITAIFA Ngasongwa: wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti...

Ngasongwa: wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji

Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Hadija  Ngasongwa amesema wawekezaji wa ndani ya nchi wanasimamiwa na sheria madhubuti zinazosimamia uwekezaji na kusaidia kuimarisha biashara nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari   julai, 4 2025 alipofanya ziara kwenye banda la viwanda na biashara katika maonyesho ya 49 ya biashara sabasaba 

“Sisi tupo hapa kutekeleza kuendeleza na kutimizaya Rais wa jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hali ya biashara nchini Tanzania,” amesema Hadija. 

Amesistiza lengo la kuanzishwa  tume ya ushindani ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda na kuhimarisha walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara nchini kati ya kampuni na kampuni, pamoja na kudhibiti bidhaa bandia.

Hadija amesema lengo kubwa ni kuhakikisha  uwekezaji ndani ya nchi waone kwamba kunasheria madhubuti ambazo zitawalinda na kusimamia uwekezaji wao wanaofanya.

“Tunajivunia na tunashukuru sana serikali kuweza kutengeneza mazingira sahihi ya wawekezaji kuhakikisha kwamba mwekezaji wa ndani kuweza kupata fursa zinazopatikana na ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri yaliyowekwa katika serikali yetu,” amesema  Hadija.

Pia ameongezea wameweza kushiriki katika maonyesho ya sabasaba ni fahari kwao na kuwaomba wageni wanaopita kwenye maonyesho kuchukua fursa zaidi ya makampuni 3000 yanayopatikana kwenye banda la viwanda na biashara.

Mwenye mtaji mdogo anaweza kupata fursa kuungana na mwenye kipato kikubwa au mwenye uwekezaji mkubwa na kuweza kuhimarisha biashara 

Aidha amesistiza kuna sheria ambayo ya kudhibiti bidhaa bandia, ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la viwanda na biashara kufika ili waweze kutofautisha bidhaa bandia na halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here