Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema shughuli za uzalishaji na uchimbaji wa mafuta na gesi wa kwenye Ajira na makampuni umeongezeka kutoka asilimia 55 hadi 85.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) Mhandisi Charles Sangwen
Hayo yamebainishwa leo Julai, 9 2025 jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba amesema hadi sasa watahakikisha shughuli zote ambazo zinaweza kutekeleza na makampuni ya Kitanzania yanafanywa na Watanzania wenyewe.
“Hii tunaipima kwa kuangalia makampuni ambayo yanekuwa yakishiriki kwenye makampuni mbalimbali ikiwemo kwenye kukusanya data kwaajili ya kuangalia mahali penye mafuta, uchimbaji wenyewe ,”amesema.
Aidha amesema kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya kuchimba visima vitatu vya Gesi asilia Mtwara ambapo ushiriki wa kampuni za kitanzania Shirika la Maendeleo ya Petrol na Gesi (TPDC) itashiriki kwa asilimia 40.
Visima hivyo vinatarajiwa kuchimbwa katika Kitalu cha Mnazi Bay kilichopo Mkoani Mtwara, ikiwa ni miaka kumi tangu kisima cha mwisho kuchimbwa katika Kitalu hicho.Uchimbaji wa visima hivyo unaotarajiwa kuanza Novemba 2025 unalenga kuongeza uzalishaji wa gesi asilia kutoka Kitalu cha Mnazi Bay kwa zaidi ya fuli za ujazo milioni 30 kwa siku.
“Katika kila makampuni 10 ambayo tunayaweka kwenye zile kazi tunahakikisha zaidi ya makampuni Sita yanekuwa ya Kitanzania,”amesema.
Amesema kwenye makampuni hayo ya nje, nafasi nyingi za watumishi hasa za juu za uongozi zinaenda nje ya nchi lakini sasa takribani asilimia 95 zinakwenda kwa Watanzania.
Aidha ameishukuru Serikali kuwa na muamko wa ushiriki wa Watanzania kwenye nafasi hizo za kazi kutokana na kuajiri watumishi kwenye nafasi kutekeleza hayo majukumu.
“Kwenye suala la Ajira Serikali ilifanya juhudi za makusudi kupitia vyuo vyetu vikuu vimekuja na gani mbalimbali ambazo wanapohitinu inakua rahisi kuwatumia katika kupata ajira,”amesema.
Akizungumzia maonesho hayo, Mhandisi Sangweni alisema Mwaka huu kimekua na maboresho ukilinganisha na miaka ya nyuma kwa kwenda kidigitali.Pia wananchi wamekuwa wengi na kutembelea kujua masuala mbalimbali yanayohusu mafuta na gesi.
Ameongeza kuwa katika maonesho hayo amebaini mwamko mkubwa wa wanaotembelea mabanda hayo upo kwenye Nishati Safi ya kupikia.
“Tunafahamu kwamba kinara wa Nishati Safi ni kinara wa nchi Kwa Afrika na Duniani, unanipa farajani kwamba Sisi watendaji wake tunaelekea maono yake kwa vitendo,”amesema.
Aidha licha ya historia ya uchimbaji wa visima vipya, mwaka 2024 Serikali iliweka historia ya kipekee kwa kuwezesha Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuongeza ushiriki wake katika Kitalu cha Mnazi Bay kutoka asilimia 20 hadi 40, hatua iliyoongeza nguvu ya kimaamuzi na ushiriki wa TPDC katika Kitalu hicho.