Home SIASA Watiania 1616 wajitokeza NLD Ubunge na Udiwani

Watiania 1616 wajitokeza NLD Ubunge na Udiwani

Na Mwandishi Wetu, TANGA

CHAMA cha Nation League for Democracy (NLD) kimetangaza idadi ya watia kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani kwaajili ya kuomba ridhaa ya Chama Chama hicho kuteuliwa kupeperusha Bendera ya Chama nchini kuwa mpaka sasa watiania wamefika 1616 huku Vijana na Wanawake wakionekana kujitokeza kwa wingi zaidi katika mchakato huo.

Katibu Mkuu wa NLD Doyo Hassan Doyo, ametangaza Julai,13 2025 kwa Waandishi wa Habari mkoani Tanga kuwa, watia nia wa nafasi ya Ubunge, Uwakilishi nchini wapo 216 na Udiwani watia nia 1400.

Amesema, zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu bado linaendelea amwishoni mwa mwezi huu ambapo tarehe 31/7/2025 ndiyo itakuwa kikomo,

” Zoezi hili bado linaendelea kwa Wanachama wajitokeze kuwania nafasi hizi za Ubunge,Uwakilishi na Udiwani,tunawaomba Wanachama na Wananchi wenye sifa za kugombea,fursa ni yao waendelee kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu,” amesisitiza

Ameongeza kuwa , upigaji Kura za maoni ni 1/8/2025 na Zoezi hilo litachukua wiki moja
kote nchini,

“Kuanzia tarehe 8/7/2025 -10/8/2025 ni kikao cha kamati kuu Taifa kwaajili ya kuteua wagombea Ubunge na wawakilishi, lakini pia kutakuwa na vikao vya Halmashauri kuu za Wilaya kwaajili ya kuwateua wagombea wa Udiwani nchi nzima” ameongeza Doyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here