Home MICHEZO Tanzania Yatangaza Utayari wa Kuandaa Mashindano ya CHAN 2025

Tanzania Yatangaza Utayari wa Kuandaa Mashindano ya CHAN 2025

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi, amesema kuwa Tanzania ipo tayari kwa ajili ya kuandaa Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), yatakayoanza rasmi Agosti 2, 2025.

Akizungumza leo Julai, 21 2025 mara baada ya ziara ya ukaguzi wa miundombinu ya michezo jijini Dar es Salaam, Dk. Yonazi alisema maandalizi yamefikia hatua nzuri na viwanja viko tayari kwa mashindano hayo makubwa.

Akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Makatibu Wakuu ya CHAN na AFCON, Dk. Yonazi alitembelea viwanja vya Benjamin Mkapa, Isamuhyo, Shule ya Sheria na Gymkhana, akisisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha miundombinu yote inakidhi viwango vya kimataifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, BGerson Msigwa, ametoa wito kwa Watanzania kuonesha uzalendo kwa kujitokeza kwa wingi viwanjani kuishangilia Taifa Stars.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here