Home KITAIFA Serikali kuleta mtoa huduma mpya wa mabasi ya mwendokasi kuondoa changamoto

Serikali kuleta mtoa huduma mpya wa mabasi ya mwendokasi kuondoa changamoto

Na Esther Mnyika,  Dar es Salaam 

SERIKALI imekiri kuwepo kwa changamoto ya uendeshwaji wa mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka( UDART ) kutoka Kimara-Kivukoni, Kariakoo na Morocco jijini Dar es salaam. Pia imesema inaondoa changamoto hiyo kwa kuleta mtoa huduma mpya atakayeleta mabasi 175  kwa mradi awamu ya kwanza.

Kauli hiyo ilitolewa leo Julai, 24 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert chalamila mara baada ya kufanya ziara fupi ya  kutembelea miradi ya barabra inayojengwa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam alisema changamoto hiyo itapungua au kumalizika kabisa baada ya mabasi hayo kuwasili.

Chalamila alisema changamoto ya usafiri huo umetokana na kuwepo kwa uchache wa mabasi tofauti ilivyokuwa awali. hivi sasa kuna mabasi 60 tu yanayotoa huduma katika njia zote zilizopo jijini hapa.

“Barabara hizi zinaendelea kwa awamu ambapo bilioni 613 zilitumika kwenye mradi huu awali kulikuwa na mabasi 200 ambayo yalikuwa yanatoa huduma kwa awamu hii ya kwanza na ndio maana wananchi walikuwa hawapati chamoto ya usafiri.

Lakini kwa sasa mabasi yaliyobaki ni 60 hivyo serikali kwa kuona changamoto hiyo imeingia ubia na sekta binafsi kwa lengo la kuendesha mradi huo ambapo hivi karibuni kampuni ya trans dar itaingiza magari 175,”amesema.

Akizungumzia mradi wa awamu ya pili kutoka gerezani hadi Mbagala  Chalamila amesema wamepata  mwekezaji mwingine atakayeleta mabasi 200 kati ya hayo 99 yanatarajiwa kufika Agosti 15 mwaka huu.

“Mabasi yanayotarajiwa kufika nchini yatakuwa marefu yenye meta 18 na yatumia mfumo wa gesi ,”amesema.

Kwa upande wa mradi wa awamu ya tatu na ya nne ujenzi unaendelea na ukikamilika tenda itatangazwa kwa lengo la kupatikana mtoa huduma .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) ,Dk.Athumani Kihamia aliwataka wamiliki wa mabasi ya daladala ambao wanatoa huduma katika maeneo yanayopita mradi wa mabasi yaendayo haraka wajisajili na wao waone namna ya kuwasaidia na kuwapatia maeneo mengine ya kutolea huduma yao.

Amesema tayari wameshazungumza na watoa huduma wapya kwa wakati wa asubuhi kila baada ya dakika tatu basi litakuwa linainhia kituoni kwa sababu muda huo wahitaji ni wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here