Na Esther Mnyika, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Nchini(TISEZA), Gilead Teri amesema Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki (EACLC) Agosti 2 mwaka huu.

Akizungumza leo Julai, 25 jijini Dar es Salaam Teri amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 282.7 hadi kukamilika.
Amesema maduka ya biashara yapo zaidi ya 2000 na kinatarajia kutoa ajira za moja kwa moja15000 na zisizo za moja kwa moja 50000.

“Kukamilika kwa kituo hichi kitasaidia kuongeza thamani ya biashara ya mauzo kwa mwaka zaidi ya shilingi bilioni 300 kwa mwaka. Pia mradi huu utaongeza ukuaji wa uchumi na bidhaa za Watanzania kupata soko nje ya nchi,”amesema.
Teri amezielekeza Halmashauri nyingine nchini kutenga maeneo kwaajili ya utekelezaji wa miradi ili kuleta uchechenuzi wa uchumi na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.
Pia amewatoa hofu wafanyabiashara kuwa kariakoo haiwezi kufa na kituo hicho hakina ushindani na kariakoo.
Ameongeza kuwa mradi huo kukuza uhusiano wa kikanda na kimataifa kutegemea wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.
Naye Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu na Uchumi kutoka Manispaa ya Ubungo, Andambike Kyomo,amesema utekelezaji wa mradi huo ukianza kwa mwaka watakusanya kodi shilingi bilioni moja.
Amesema wakazi wa wilaya hiyo niwanufaika moja kwa moja kwa sababu mapato yanayopatikana hapo kutoa huduma kwa wananchi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kituo hicho, Cathy Wang amewataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya uwepo wa kituo hicho.
Amesema kituo hicho ni muhimu kilichoanzishwa ili kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kikanda.
“TISEZA na Manispaa ya Ubungo zimesaidia kutoa muongozo wa kisera na wawekezaji motisha ambazo zimehahakisha mpango huo unawiana kikamilifu na dira ya Tanzania,”amesema.
Utekelezaji wa kituo hicho ulianza Mei 2023 na umekamilika mwaka huu.