Home KITAIFA Nchi 10 kujadili mbegu za wakulima

Nchi 10 kujadili mbegu za wakulima

Na Mwandishi Wetu

WADAU wa mbegu za wakulima kutoka nchi 10 duniani kesho watakutana nchini Tanzania kujadiliana muhimu wa mbegu hizo na sera.

Hayo yamebainishwa leo Julai, 27 2025 na Mratibu wa Kikosi Kazi cha Mbegu (SWG), Daud Manongi wakati akizungumza na mwandishiwa habari hii.

Manongi amesema warsha hiyo ya siku tatu itahusisha wataalam wa kilimo, wakulima na serikali kutoka nchi 10 ambazo zimeweka kipaumbele kwenye mbegu za wakulima.

“Warsha hii inahusisha wawakilishi kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Zimbabwe, Ethiopia, Mali, Senegal, Italia, na Uswisi ambapo watajikita kujadili mifumo jumuishi ya mbegu,” amesema.

Manongi amesema warsha muhimu ya kisera itakayolenga kutambua mchango wa mbegu za wakulima katika sheria na kanuni za mbegu nchini Tanzania.

Amesema warsh hiyo imeratibiwa na Shirika la SWISSAID kwa kushirikiana na Mtandao wa Baionuwai Tanzania (TABIO) kama mshirika anayeongoza utekelezaji wa kazi za kisera, wajumbe
wa SWG, Alliance for Food Sovereignty in Africa (AFSA) ikitajwa kama mshirika muhimu wa muungano wa CROPS4HD na Wizara ya Kilimo.

Manongi amesema warsha hiyo ina kauli mbiu ya “Kutoa nafasi kwa mbegu za wakulima kwenye Kanuni za Mbegu Kujifunza kutoka Ulimwenguni na Kubaini Njia kwa Tanzania,”amesema.

Tukio hili linafanyika kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Kilimo, na linawaleta pamoja wadau kutoka sekta ya mbegu, wataalamu wa sera, wawakilishi wa wakulima, na taasisi za kitaifa na kimataifa.

Amesema hilo si suala la kitaalamu tu ni kuhusu usalama wa chakula, urithi wa wakulima, na uhuru wao.

“Ikiwa sera za mbegu zitaendelea kuunga mkono mbegu za makampuni pekee, tutapoteza aina za mbegu zenye umuhimu wa kihistoria na kisayansi kwa jamii zetu.

Lengo letu ni kuhakikisha kwamba mfumo wa mbegu unakuwa jumuishi—na unaotambua pia nafasi ya wanawake kama wahifadhi wakuu wa mbegu asilia. Pia tunataka kuona mbegu za wakulima zikifikia wakulima kwa njia rasmi, kupitia maduka ya pembejeo,”ameeleza.

Mratibu wa TABIO, Abdallah Mkindi, alisema mkutano huo ni hatua muhimu katika mustakabali wa mbegu na kilimo nchini.

“Mbegu zinazohifadhiwa na wakulima zimekuwa chanzo cha chakula, ustahimilivu na utamaduni kwa vizazi. Zimezoea mazingira ya wenyeji na ni suluhisho la kweli dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”

“Kupitia warsha hii, tunalenga kubuni mazingira ya kisera yatakayotoa nafasi kwa mifumo yote miwili ya mbegu rasmi na isiyo rasmikushirikiana kwa njia ya usawa,” amesema.

Mkindi amesema wanaishukuru Wizara ya Kilimo kwa utayari wake wa kushiriki majadilianona akaipongeza SWISSAID kwa kuratibu warsha hiyo pamoja na AFSA kwa mchango wake kupitia muungano wa CROPS4HD.

Amesema mbali na Wizara ya Kilimo na TABIO, warsha hii imeunhwa mkono na wadau wengine ambao ni ESAFF Tanzania, PELUM Tanzania, ILES DE PAIX (IDP), SHIWAKUTA, DMDD na Agroecology Hub ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) na mashirika mengine mengi yanayofanya kazi na wakulima moja kwa moja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here