Home UCHUMI Dk. Mpango aipongeza BoT kwa kutengeneza Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS)

Dk. Mpango aipongeza BoT kwa kutengeneza Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS)

Na Esther Mnyika, Dar es Salaam

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) pamoja na wataalamu wake waliotengeneza Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS) wenye viwango vya kimataifa na kwa gharama nafuu ikilinganishwa na bei za mifumo kama hiyo kwenye soko la kimataifa.

Dk.Mpango amesema hayo leo Julai, 30 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS) Amasema BoT imekuwa taasisi ya kwanza Barani Afrika kuunda Mfumo huo ambapo jumla ya shilingi bilioni 81.32 zimeokolewa kwa kutumia wataalam wa ndani na kuongeza ufanisi wa Benki Kuu katika kusimamia ufanyikaji wa miamala pasipo vizuizi.

“BoT kwa kushirikiana na taasisi husika, kama Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Wakala wa Serikali Mtandao (e-GA) na Wizara zinazohusika, kuhakikisha wanasimamia vema Mfumo wa iCBS na mifumo mingine yote ya malipo, ili kuendelea kupata matokeo stahiki katika maendeleo ya uchumi wa nchi,”ameagiza.

Amesisitiza zaidi kuhusu kujikita kwenye matumizi sahihi ya mifumo ya kidijitali katika kufanya miamala na malipo mbalimbali, ili kupunguza matumizi ya fedha taslimu.

Dk.Mpango ametoa rai kwa Benki Kuu ya Tanzania kuhakikisha wanadhibiti na kuchukua hatua stahiki kwa wimbi la wakopeshaji kupitia mitandao ya simu na kuhakikisha wananchi hawaendelei kutapeliwa.

Aidha ameitaka Benki Kuu kuendelea kutoa elimu kwa Umma juu ya athari za kurubuniwa na matapeli hao na fursa sahihi za kupata mikopo nafuu katika Mabenki.Wakopeshaji hao wanatoza riba kubwa, wanaingilia faragha za watu na hata kusambaza taarifa za wakopaji wao bila ridhaa.

Ametoa wito wa kuhakikisha ulinzi wa hakimiliki ya Mfumo wa iCBS na kusisitiza umuhimu wa kushirikiana na taasisi na mifumo ya ulinzi wa miliki bunifu, kutekeleza jambo hilo ili kukuza utamaduni wa ubunifu nchini.

Aidha, ametoa wito kwa Wizara zote, kuongeza motisha kwa wabunifu wa ndani ambao wana mchango mkubwa katika kuokoa fedha za kigeni na kuongeza tija kwa ujumla.

Amesema Serikali kwa upande wake itaendelea kuchukua hatua zaidi za kuimarisha mazingira ya utafiti na ubunifu ikiwa ni pamoja na kuongeza fedha za utafiti, kuanzisha vituo vingi vya ubunifu na vituo atamizi pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za elimu ya juu, serikali, na sekta binafsi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande alisema sio jambo la kawaida mfumo kuujenga Watanzania wenyewe ambao Tanzania ni ya kwanza Afrika kwa kuwa na mfumo huo jumuishi

Amesema ni historia kwa Tanzania kuingia katika mfumo huo Afrika hivyo Gavana Emmanuel Tutuba kwa hilo na mfumo huo unahitaji ulinzi mkubwa ubaki kuwa salama na Watanzajia wauthamini.

“Moja ya changamoto iliyofanyika juko nyumba jambo lilofanywa na wazawa huwa halina maana hivyo lazima uthamink cha kwako kwani ndipo maendeleo yanapopatikana,”amesema.

Naye Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Jerry Silaha ameipongeza BoT kwa mfumo jumuishi unaosimamia sekta ya fedha na kutekeleza maagizo ya Rais Samia kutaka mifumo isomane.

“Hadi sasa jumla ya mifumo 898 inasomana huku 514 ikiwa ya serikali na 384 sekta binafsi na kwa sekta ya fedha ni BoT pekee.

Waziri wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Saada Mkuya amesema mfumo huo.umekuwa suluhisho ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili awali na Zanzibar ni wanufaika kwaji ufanisi wa mabenki umeongezeka.

“Hakuna kipindi BoT imekuwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama kipindi hiki kuboresha mifumo ya huduma za kifedha, na kufanikiwa kutatua changamoto za maduka ya fedha za kigeni na kuweka mazingira mazuri ya biashara hiyo,” amesema.

Kwa upande wake, Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba amesema mfumo huo umetengenezwa na wataalamu wa benki hiyo ambao umegharimu shilingi bilioni 10.63.

Amempongeza Rais Dk. Samia kwa kuwezesha mifumo hivyo wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza falsafa ya 4R kuimarisha uwekezaji, kuongeza ukwasi na kuimarisha thamani ya shilingi.

Amesema uchumi wa Tanzajia umeendelwa kufanya vizuri japo ya kuwepo na changamoto za kidunia iikiwepo mabadiliko ya tabia nchi.

Amesema mfumo huo ni wa kisasa na nyeti kwanza utasaidia kuondoa makosa ya kibinadamu na kuongeza usahihi na kuondoa changamoto katika mifumo wa kidigitali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here