Home KITAIFA Waandishi wa habari kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29

Waandishi wa habari kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewasisitiza Waandishi wa Habari  kuandika habari zenye kuhamasisha na kuelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu na kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu.

Hayo ameyasema leo Agosti,  2 2025 Jijini Dar es  na Mwenyekiti INEC, Jaji (Rufani), Jacob Mwambegele wakati akifungua mkutano wa Kitaifa wa INEC na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema uchaguzi wa mwaka huu umebeba kauli mbili ya “Kauli mbiu ni Kura Yako, Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura”

“Waandishi ni daraja muhimu baina ya wananchi na Tume pia ni wadau muhimu katika eneo hili na kiungo muhimu kwenye uchaguzi Mkuu,” amesema.

Amesema umuhimu wa kufanya  kikao  hicho cha pamoja ni kubadilishana uzoefu  wa uchaguzi  kuepusha  dosari ambazo zitaathiri uchaguzi na kujadiliana namna ya kufanya kazi katika kipindi hichi.

Jaji Mwambegele amesema ratiba ya uchaguzi Ibara ya 41 kifungu kidogo cha 4 na Ibara ya 49 ya Katiba ya Tanzania inatoa fursa kwa INEC kusimamia uchaguzi.

“Fomu za Urais zitaanza kutolewa Agosti 9 hadi 25 na wabunge itakuwa Agosti 14 hadi 27.Kampeni zitaanza Agosti 28 kumalizika Oktoba 27 Zanzibar  na  Agosti,  28 Tanzania Bara kumalizika Oktoba 28 hivyo vyama vitafanya kampeni kwa kufuata sheria na katiba ya nchi,” ameeleza.

Pia ameviomba vyombo vya habari kutumia nafasi yake kutoa elimu ili vyama viweze kushiriki kwa weledi na usahihi.

Aidha amesema INEC imetunga kanuni za uchaguzi za 2025 ambazo zinaelekeza namna vyombo na vyama vya siasa vinapaswa kufanya kazi kwa matakwa ya kisheria.

Amesema uchaguzi huo utahusisha wa majimbo 272 yatashiriki uchaguzi na majimbo 222 ni ya Tanzania Bara na Zanzibar majimbo 50 kuna ongozeko la Majimbo nane na  kata za 3960 kufanya uchaguzi wa madiwani zitashiriki uchaguzi huo wa Oktoba 29 mwaka huu.

Jaji Mwambegele amesema INEC imejipanga kutoa elimu ya mpiga kura kwa njia mbalimbali kama vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, magari ya matangazo, matamasha na taasisi 164 zitashiriki pia utoa elimu.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti  wa INEC, Jaji (Rufani) Mstaafu Mbarouk S Mbarouk  amesema  Tume hiyo inaimani na waandishi wa habari na wadau mbalimbali katika kuhamasisha  uchaguzi. 

Amesisitiza waandishi wa habari kufanya hamasa kubwa kwa wananchi  waweze kupiga kura ili wachague viongozi wanaowataka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here