Home KITAIFA Wizara ya Nishatina taasisi zake zashiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Dodoma

Wizara ya Nishatina taasisi zake zashiriki maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Dodoma

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WIZARA ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki Katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ambayo yameanza Agosti, 1 2025 Katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma.

Maonesho hayo yamebebwa na kaulimbiu iya ” Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025″,

Katika maonesho hayo ambayo yamefunguliwa na Makamu wa Rais, Dk. Philip Isdor Mpango, Watalaam wa Wizara pamoja na kueleza mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Nishati ikiwemo ukamilishaji wa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na Usambazaji wa Umeme Vijijini, wanatoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia.

Aidha wananchi wanafahamishwa kuhusu mipango mbalimbali ambayo Wizara imepanga kutekeleza katika mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kusambaza umeme vitongojini na utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Taasisi za Wizara ya Nishati zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania ( TGDC).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here