Home KITAIFA Wananchi wakaribishwa banda la Wizara ya Nishati Nanenane Dodoma

Wananchi wakaribishwa banda la Wizara ya Nishati Nanenane Dodoma

📌 Kufahamu fursa na miradi inayoendelea kutekelezwa

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WIZARA ya Nishati imeendelea kukaribisha wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima (NANENANE) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Fredrick Marwa, Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati amesema katika maonesho hayo leo Agosti, 4 2025 Wizara inaeleza kuhusu kazi mbalimbal zinaoendelea kufanyika ikiwemo za utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Bonde la Eyasi Wembere.

Marwa amesema wananchi watakapofika katika Banda la Wizara ya Nishati pia watajionea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Wizara pamoja na Taasisi zake ikiwemo TANESCO, EWURA, REA na TPDC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here