Home KITAIFA Wananchi wakaribishwa Nanenane kufahamu kwa kina mpango mahsusi wa Nishati 2025-2030

Wananchi wakaribishwa Nanenane kufahamu kwa kina mpango mahsusi wa Nishati 2025-2030

📌 Ni uliosainiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300

Na Mwandishi wetu, Dodoma

WIZARA ya Nishati imekaribisha wananchi kuendelea kutembelea Banda la Wizara ya Nishati katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima- NANENANE jijini Dodoma ili kufahamu masuala mbalimbali ikiwemo Mpango mahsusi wa Taifa wa Nishati wa mwaka 2025-2030.

Imeelezwa kuwa mpango huo uliosainiwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300 mwezi Januari 2025 unalenga kuunganisha umeme kwa wananchi milioni 8.3 ifikapo 2030 na kufikisha nishati safi ya kupikia kwa asilimia 75 ya Watanzania ifikapo 2030.

Mpango huo pia unalengai kiwemo kuongeza upatikanaji wa umeme na kuongeza ushiriki wa nishati jadidifu katika uzalishaji wa umeme.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here