Na Mwandishi wetu, Dodoma
MFANYABIASHARA wa Njiwa wa Mapambo Nchini, Abdulaziz Almasi amawataka watanzania kuingia kwenye biashara hiyo kwa sababu kuna fursa mbalimbali.

Hayo ameyasema leo Agosti, 6 2025 kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane jijini Dodoma Almasi amesema ameleta aina 10 za njiwa ambao ni mapambo kwenye maonesho hayo ambao wanaanzia bei shilingi laki nne hadi milioni moja.
Amesema njiwa unaweza kufuga kwa malengo mbalimbali ikiwemo wa mapambo, nyama na kuna aina nyingi za njiwa.
“Njiwa ambao nafuga mimi asilimia kubwa wanatokea nchini Marekani japo kuna njiwa wa notokea nchini German na sehemu zingine hivyo biashara ya njiwa ni fursa nawakaribisha kwenye fursa hii,”amesema.

Amesema chakula cha njiwa hao ni mtama, choloko na uwele nijwa wanafaida kubwa na wanazaliana kwa wingi
Almasi ameeleza kuwa amefanya biashara ya njiwa zaidi ya miaka 15 alianza kufuga njiwa sita hadi sasa nina njiwa 96 wa mapambo ukiachana na njiwa wa kawaida.
“Changamoto kubwa nilinayo ni watu kushaangaa gharama ya njiwa ukiona njiwa alivyo gharama yake ni shilingi milioni moja njiwa wa mapambo wa gharama biashara hii ni fursa,” amesema.
Ameongeza kuwa njiwa wa mapambo wana thamani kubwa hasa wale wa ranging adieu au za kifahari