Na Mwandishi wetu, Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Abdul Mombokaleo ameipongeza Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake kwa ubunifu katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane.

Hayo ameyasema Mombokaleo baada ya kutembelea banda la Wizara hiyo pamoja na mabanda na taasisi hizo yaliyopo kwenye maonesho hayo jijini Dodoma ikiwa lengo ni kujua majukumu mbalimbali yanayofanywa.
Amesema sekta ya uchukuzi ni mhimili muhimu katika kufanikisha maendeleo ya kilimo, biashara na uwekezaji nchini.

“Nimepata maelezo juu ya elimu inayotolewa na wadau wa Viwanja vya Ndege pamoja na marejesho kutoka kwa wadau ili kuangalia namna ya kuboresha zaidi shughuli za uendeshaji katika viwanja hivi,”amesema.

Aidha Mombokaleo alitembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa lengo la kupata ufahamu juu ya utendaji kazi wa mitambo ya kuzima moto katika majengo marefu ikumbukwe TAA inafanya kazi kwa ukaribu na Jeshi hilo.