Home SIASA CCM Mkoa wa Dar es Salaam yatangaza Majina ya wagombea wa...

CCM Mkoa wa Dar es Salaam yatangaza Majina ya wagombea wa udiwani

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

KATIBU wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga,ametangaza majina ya uteuzi wa wagombea nafasi ya udiwani na viti maalum Mkoa Dar es Salaam.

Majina hayo yametangazwa leo Agosti 14,2025 jijini Dar es Salaam mara baada ya zoezi hilo kukamilika kwa mchakato wa kura za maoni na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kujadili na kufanya uteuzi wa mwisho ya wagombea watakaokwenda kukiwakilisha Chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu.

Aidha ,amesema kwamba kwa ujumla kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam kiliazimia na kuteua kwa asilimia 99.2 wagombea waliongoza kwenye kura za maoni katika kata zote 102.Hata hivyo,katika kata ya Vijibweni kutokana na changamoto mgombea aliyeongoza kura za maoni hakuteuliwa hivyo kufanya asilimia 0.98 ya waliongoza kura za maoni kutoteuliwa.

“Uteuzi huu umezingatia Kanuni za uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola,Kanuni ya 9(1) inayosema”Mgombea yoyote wa CCM anayetaka kuingia katika chombo Cha Dola,atateuliwa kwa kuzingatia kura za maoni zilizopigwa.

Mgombea atakayeteuliwa ni yule anayeongoza kwa wingi wa kura za maoni alizopata.Isipokuwa kwamba endapo itathibitika kuwa kura hizo za ushindi amezipata kwa njia ya rushwa,kikao Cha uteuzi wa mwisho hakitamteua mgombea nafasi aliyoomba”,amesema Bananga.

Hata hivyo,ametaja mchanganuo wa uteuzi wa wagombea katika Wilaya 5 na kata 102 za Mkoa wa Dar es Salaam

Pia amesema kwamba uteuzi wa wagombea walioteuliwa ni asilimia 50.98 ni ya wagombea wapya na asilimia 49.02 ni ya wagombea wa zamani kwa hiyo mchakato huu umezingatia demokrasia ndani ya Chama Cha Mapinduzi

Sambamba na hayo katika uteuzi wa wagombea Wilaya ya Ilala ina majimbo manne Kata 36 katika Jimbo la Ilala Lina Kata 10 wameteuliwa wagombea wa zamani ni saba na wapya wagombea watatu.

Pia ametaja Jimbo la Kivule Kata ziko sita wagombea wa zamani watatu na wagombea wapya watatu na Katika Jimbo la Ukonga lina kata saba wagombea wa zamani ni mmoja na wagombea wapya sita.

Ameongeza kwamba Jimbo la Segerea ziko kata 13 wagombea walioteuliwa wa zamani ni saba na wagombea wapya sita pamoja na kusema kuwa Wagombea wa Udiwani Viti Maalum wako 14 .

Aliendelea kwa kutaja majina Wilaya ya Temeke Kata 23 kwa kusema kuwa Jimbo la Temeke Kata 13 wagombea wa zamani ni 11 na wagombea wapya wawili na kwa upande wa Jimbo la Mbagala Lina kata sita wagombea wote ni wapya.

Jimbo la Chamazi Lina kata nne wagombea wapya watatu na mmoja wa zamani ambapo Jimbo la Kigamboni lenye kata tisa wagombea wapya tatu na wazamani sita.

Alithibitisha katika Wilaya ya Ubungo Lina Kata 14 ambapo Jimbo la Ubungo Kata nane wagombea wa zamani wanne na wapya wanne ,aidha Jimbo la Kibamba Kata sita na wagombea sita wote wapya.

Alimalizia kwa kutaja wagombea walioteuliwa kataka Wilaya ya Kinondoni yenye Kata 20 ambapo katika Jimbo la Kinondoni lina kata 10 wagombea wa zamani watano na wapya watano na Jimbo la Kawe lina Kata 10 wagombea wa zamani wawili na wagombea wapya ni nane.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here