Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Mohammed Ali Kawaida, (MCC) amezindua rasmi Kijani Ilani Chatbot, mfumo wa kidijitali utakaowasaidia vijana kupata taarifa kuhusu utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025 na mipango ya 2025-2030.

Akizungumza Agosti, 25 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi huo, Kawaida alisema chatbot hiyo inalenga kuwapa vijana majibu ya moja kwa moja kuhusu maendeleo na ahadi za chama, na kuwahamasisha kutumia teknolojia kwa manufaa ya taifa.
“Kijani Ilani Chatbot itakwenda kutuonyesha ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2025-30 vitu gani imehahidi hususani kwa upande wa vujana wa kitanzania” amesema Kawaida.

Aidha amewasihi vijana kutumia Mfumo wa Kijani Ilan Chatbot kikamili katika kupata majibu yote ya maswali kuhusu ilani na utekelezaji wake na kupata taarifa na kukuza uelewa.
“Twendeni tukatumie mfumo huo ili kuondoa upotoshaji unaofanywa na watu wasiokuwa na mapenzi mema na taifa letu kwa kuwaambia na kuwaonyesha watanzania Ukweli” ameongeza kawaida.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa (UVCCM) Taifa, Halid Mwinyi amesema mfumo huo utawezesha mawasiliano ya Moja kwa Moja ambapo mtumiaji ataweza kuliza maswali na kupokea majibu kwa haraka na njia rahisi pamoja na kijifunza kuhusiana na uchaguzi na ilani ya ccm.
Ameongeza kuwa Mfumo utaleta mambo yafuatayo hususani kutoa taarifa kwa haraka, sahii naza kidigital kuhusu ilani ya ccm, miradi ya maendeleo na namna jamii inavyonufaika husani vijana.

“Kuwezesha vijana kuliza maswali na majibu ya moja moja kwa kupitia mfumo huu na kuongeza vijana kuhusu nafasi yao katika maendeleo ya taifa na ushiriki wa kisiasa, kukuza matumizi ya kitekonlojia kuhusu akili mnemba katika elimu ya siasa na utawala bora” amesema mwinyi
Ameongeza kuwa mfumo huo utawezesha vijana kuuliza maswali na kupata taarifa sahihi kuhusu siasa, uchaguzi, na nafasi yao katika maendeleo ya nchi.