Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
CHAMA cha National League for Democracy (NLD) kinapenda kuwataarifu wananchi, na wanachama wake, vyombo vya habari kuwa Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 zitafanyika mkoani Tanga, katika Viwanja vya Stendi ya Mabasi ya Pangani, siku ya Jumatano, tarehe 4 Septemba 2025, kuanzia saa 8:00 mchana.

Katika uzinduzi huo, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Doyo Hassan Doyo, pamoja na Mgombea Mwenza, Chausiku Khatibu Mohamed, wanatarajiwa kuhutubia wananchi na kueleza kwa kina sera na vipaumbele vya ilani ya uchaguzi ya NLD kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Aidha, viongozi wakuu wa chama, wagombea ubunge, na wagombea udiwani kutoka mikoa mbalimbali nchini watashiriki katika tukio hilo kubwa la kihistoria na la kisiasa.
Wakazi wa mkoa wa Tanga na mikoa jirani mnakaribishwa kwa wingi kuhudhuria uzinduzi huo wa kampuni ili kupata fursa ya kusikiliza sera mbadala zinazolenga kuleta maendeleo, na ustawi wa Mtanzania kwa ujumla.