Home SIASA Dk. Mwinyi achukua fomu ya urais Zanzibar

Dk. Mwinyi achukua fomu ya urais Zanzibar

Na Mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Agosti, 30 2025 amechukua fomu ya uteuzi wa kuwania kiti cha Urais wa Zanzibar katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Dk. Mwinyi ameambatana na Mke wake Mama Mariam Mwinyi pamoja na familia na viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Dk.Mohamed Said Dimwa pamoja na wanachama na wakereketwa wa maendeleo waliokusanyika kwa wingi kushuhudia hatua hiyo muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here