Home KITAIFA Mkurugenzi wa uchaguzi washuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Act-Wazalendo

Mkurugenzi wa uchaguzi washuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Act-Wazalendo

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Ramadhani Kailima, (kulia) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Adam Mkina wakishuhudia ubandikaji wa fomu za uteuzi za Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – WAZALENDO), Luhaga Joelson Mpina na Mgombea Mwenza, Fatma Abdulhabib Ferej majira ya Saa 10:00 jioni ya leo Septemba, 13 2025.

Ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria inayotaka fomu hizo kubandikwa kwa Saa 24 ili kutoa fursa ya kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi wa mgombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais ambapo pingamizi hilo linaweza kuwekwa na mgombea mwingine, Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here