Home KIMATAIFA Malawi kupiga kura leo, ushindani watarajiwa kati ya Rais Chakwera na Mutharika

Malawi kupiga kura leo, ushindani watarajiwa kati ya Rais Chakwera na Mutharika

Lilongwe, Malawi

Malawi inaelekea kwenye uchaguzi leo, Jumanne, utakaomkutanisha Rais Lazarus Chakwera na mtangulizi wake, Peter Mutharika, huku taifa hilo likikabiliwa na mfumuko wa bei uliokithiri na uhaba wa mafuta.

Jumla ya wagombea 17, akiwemo rais wa zamani Joyce Banda, wanawania urais, lakini wachambuzi wanatarajia kinyang’anyiro kikali zaidi kati ya Chakwera, mwenye umri wa miaka 70, na Mutharika, mwenye miaka 85. Endapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura, uchaguzi utaingia katika duru ya pili.

Malawi, yenye takriban watu milioni 22, imekumbwa na mdororo wa kiuchumi tangu Chakwera kuchaguliwa mwaka 2020, hali iliyochochewa na athari za kimbunga kikali na ukame ulioathiri taifa hilo.

Kashfa za ufisadi pia zimechangia kutoridhishwa na pande zote mbili. Chakwera aliingia madarakani akiahidi kupambana na ufisadi uliodaiwa kushamiri wakati wa utawala wa Mutharika, lakini usimamizi wa kesi hizo umekosolewa kwa upendeleo na kuchelewa.

Mbali na kumchagua rais, Wamalawi pia wanawapigia kura wabunge na madiwani wa mitaa leo Jumanne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here