Home KIMATAIFA Trump: Sikuarifiwa mapema kuhusu shambulizi la Israel nchini Qatar

Trump: Sikuarifiwa mapema kuhusu shambulizi la Israel nchini Qatar

Washingtona, Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Jumatatu kwamba hakujulishwa mapema na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, kuhusu shambulizi la anga la Israel nchini Qatar wiki iliyopita.

Kauli ya Trump inakuja baada ya ripoti ya Axios kudai kuwa Netanyahu alimfahamisha Rais wa Marekani muda mfupi kabla ya shambulizi hilo kutekelezwa.

Kwa mujibu wa utawala wa Trump, taarifa rasmi zilipokelewa baada ya makombora kurushwa, hali iliyomnyima fursa ya kupinga hatua hiyo ya kijeshi. Hata hivyo, Axios ilinukuu maafisa wa Israel wakisema Ikulu ya Marekani iliarifiwa mapema, ingawa muda wa kuzuia shambulizi hilo ulikuwa mdogo.

Shambulizi la anga la Israel lililenga kuwaua viongozi wa kisiasa wa Hamas waliokuwa nchini Qatar, na limeibua ukosoaji mkubwa Mashariki ya Kati na kwingineko, huku likionekana kuongeza wasiwasi katika eneo linalokumbwa na changamoto za kiusalama.

Awali, Trump alikanusha kuhusika na uamuzi wa Israel kushambulia Qatar. Alipoulizwa Jumatatu iwapo Netanyahu alimjulisha moja kwa moja kabla ya operesheni hiyo, alijibu: “Hapana, hapana, hawakunijulisha.”

Ofisi ya Netanyahu ilisisitiza baada ya ripoti ya Axios kwamba shambulizi hilo lilikuwa operesheni “huru kabisa” ya Israel.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here