Home KIMATAIFA Mshukiwa wa mauaji ya Charlie Kirk akiri kwa ujumbe, akabiliwa na mashtaka...

Mshukiwa wa mauaji ya Charlie Kirk akiri kwa ujumbe, akabiliwa na mashtaka saba

Utah, Marekani

Mwanamume anayedaiwa kumpiga risasi na kumuua mwanaharakati wa mrengo wa kulia, Charlie Kirk, ameripotiwa kukiri tendo hilo kupitia ujumbe aliomuandikia mpenzi wake, waendesha mashtaka wamesema.

Tyler Robinson (22) alieleza kwa maandishi kuwa aliuwa Kirk, akiacha barua chini ya baobonye ili mpenzi wake aipate. “Nilipata fursa ya kumuondoa Charlie Kirk, na nimeitumia,” barua hiyo ilisomeka kwa mujibu wa Wakili wa Kaunti ya Utah, Jeffrey Gray.

Waendesha mashtaka pia wamewasilisha ujumbe wa maandishi kati ya Robinson na mpenzi wake, ikiwemo mmoja uliodai kuwa alimpiga risasi Kirk kwa sababu “anamchukia sana.”

Kwa sasa mshukiwa anazuiliwa bila dhamana katika kitengo maalum cha makazi gerezani na alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Jumanne.

Anakabiliwa na mashtaka saba: mauaji ya kuchochewa, kumiliki silaha kinyume cha sheria, makosa mawili ya kuzuia haki, makosa mawili ya kuharibu ushahidi na kufanya uhalifu wa kutumia nguvu mbele ya watoto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here