Home KIMATAIFA Polisi Somalia wawakamata wafuasi wa TikTok kwa kumtusi Rais Mohamud

Polisi Somalia wawakamata wafuasi wa TikTok kwa kumtusi Rais Mohamud

Mogadishu, Somalia

Polisi nchini Somalia wamewakamata vijana wanne wanaotumia mtandao wa TikTok kwa madai ya kumtusi Rais Hassan Sheikh Mohamud kupitia video ya densi.

Katika video hiyo, washukiwa walionekana wakicheza wimbo wa kampeni uliotumika kwenye uchaguzi wa mwaka 2022, lakini wakiubadilisha maneno na kujumuisha lugha ya matusi.

Taarifa ya polisi imesema washukiwa hao wako kizuizini na watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka. Hata hivyo, hawajazungumza chochote tangu kukamatwa kwao.

Somalia imekuwa ikishuhudia hatua za vyombo vya usalama dhidi ya washawishi wa mitandao ya kijamii wanaochapisha maudhui yanayoonekana kuwa ya uchochezi, matusi ya koo au uasherati. Lakini hii ni mara ya kwanza watu wanakamatwa kwa madai ya kumtusi kiongozi mkuu wa nchi kupitia TikTok.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here