Home UCHUMI BOT yang’ara Kimataifa yapewa tuzo kwa huduma jumuishi za fedha

BOT yang’ara Kimataifa yapewa tuzo kwa huduma jumuishi za fedha

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

BENKI ya Kuu ya Tanzania (CCM) imetunukiwa Tuzo Kuu ya ubunifu katika Huduma Jumuishi za Fedha (Nestor Espenilla Jr. Financial Inclusion Innovation Award) inayotolewa naJumuiya ya Huduma Jumuishi za Fedha (AFI) yenye nchi wanachama 84.

Tanzania ni mwanachama wa taasisi hiyo kupitia Benki Kuu kuanzia mwaka 2011Tuzo hiyo iliyopokelewa na Naibu Gavana anayeshughulikia udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Sauda Msemo, kwa niaba ya Gavana wa BoT Emmanuel Tutuba, wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Huduma Jumuishi za Fedha uliofanyika mjini Swakopmund, nchini Namibia mwanzo mwa mwanzoni mwa 2025.

Akionyesha tuzo hiyo Septemba,16 2025 jijini Dar es Salaam waandishi wa habari Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Lucy Shaidi amesema baadhi ya mambo yaliyofanya benki kuu kutunukiwa tuzo hiyo ni pamoja na utekelezaji madhubuti wa mfumo wa malipo yapapo kwa papo yaani TIPS na namna ambavyo umesaidia kupunguza gharama kwa wananchi kufanya miamala kwanjia ya kidigitali.

Vilevile Benki Kuu imeongesha mafanikio katika matumizi ya msimbo milia wa malipo(QR Code) unaofahamika kama TANQR unaowezesha wafanyabiashara nchini kupokea malipo ya bidhaa na huduma kwa njia rahisi kutoka kwa benki na kampuni zasimu.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi, Kurugenzi Mifumo ya Malipo ya Taifa Mutashobya Mushumbusi, amesema benki kuu ya Tanzania ni kinara katika ubunifu wa huduma za kifedha katika nchi 84 wananchama kutoka bara la Afrika na Asia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here