*Asema ni uwanja utakaotumika na timu za Mataifa mbalimbali kwenye maandalizi ya AFCON 2027
Na Mwandishi wetu, Arusha
MKUU wa mkoa wa Arusha CPA Amos Gabriel Makalla amempongeza Mkurugenzi wa Black Rhino Academy Foundation ya Mjini Karatu, Nickson Marick kwa uwekezaji mkubwa wa shule na uwanja wa kisasa ambao utakuwa sehemu ya viwanja vizuri vitakavyotumiwa kwa maandalizi kwa Timu zitakazoshiriki mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2027.

CPA Makalla ameyasema hayo Septemba 22, 2025 Mjini Karatu kwenye ziara yake ya Kikazi Wilayani Karatu ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea shule hiyo ya kimataifa na uwanja huo wa michezo unaomilikiwa na Taasisi ya Black Rhino.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Black Rhino Foundation,Nickson Marick amemshuru Mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kutembelea Taasisi yao akiahidi kuwa uongozi wa Black Rhino Foundation upo tauyari kutoa ushirikiano kwa serikali kuelekea kufanikisha michuano ya AFCON inayotarajiwa kuchezwa mwaka 2027 chini ya uenyeji wa pamoja kati ya Mataifa ya Tanzania, Kenya pamoja na Uganda na kushirikisha timu za Taifa kutoka Barani Afrika.