Na Esther Mnyika, Zanzibar
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itahakikisha hospitali zote zinatoa huduma za kibingwa ikiwemo Hospitali ya Abdallah Mzee kupatiwa mashine ya MRI.

Akizungumza Septemba,24 2025 Dk. Mwinyi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Makombeni,Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba amesema kasi ya maendeleo yaliyopatikana katika kipindi vha miaka mitano iliyopita itongezeka zaidi kupitia miradi mikubwa ya maendeleo.
“Serikali italeta mashine ya MRI hapa hapa pemba mashine ya kusafisha damu ma figo kuletwa pemba hakuna watu kusafiri kwenda Dar es Salaam au nje ya nchi kupata huduma hapa hapa na kuhakikisha mnapata huduma bora,” amesema.

Akizungumzia kuhusu zao la karafuu Dk. Mwinyi amesema serikali itaendelea kulipa kipaumbele zao hilo ikiwa ni zao kuu la uchumi na kuliongezea thamani.
“Bei ya karafuu haijabadilika na haitabadilika asilimia 20 inachukua serikali kwaajili ya huduma na asilimia 80 anachukua mkulima hivyo zao la karafuu tutaendelea kulienzi na linahitajika duniani,”amesema.

Ameongeza kuwa akipewa ridhaa ya kuwa rais kipaumbele cha kwanza itakuwa ajira kwa vijana serikali kuhakikisha vijana wengi wanapata ajira serikali, sekta binafsi na kujiajiri.
Dk. Mwinyi amesema uchumi wa bluu ni sekta mama hivyo kutoa mikopo kwa wakulima wa mwani na wavuvi na boti kwaajili ya shughuli zao mbalimbali.

“Hivi karibuni serikali inatarajia kuleta boti mbili za kisasa kwaajili ya Unguja, pemba na Tanga na meli ya Mv mapinduzi 2 tayari kuzinduliwa hivi karibuni, ” amesema.

Dk.Mwinyi amewataka Wanzabar kuepuka siasa za kikanda, kidini, ubaguzi na mifarakano amani na mshikamano ni nguzo kuu za maendeleo

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kudumisha amani, maridhiano na mshikamano ili kutekeleza mipango ya maendeleo yenye manufaa kwa wananchi wate.